Kozi Fupi

Utangulizi

Kozi fupi ni kozi zinazotolewa katika vyuo vya ufundi stadi katika kipindi cha mwezi mmoja hadi miezi sita na huo muda wa kozi unategemea mahitaji ya fani husika. Kozi za muda mfupi hutolewa katika vipindi mbalimbali vya mwaka.

Orodha ya kozi za muda mfupi zinapatikana kwenye vyuo vya VETA na huratibiwa na vyuo husika ambapo fomu za kujiunga zinapatikana kwenye vyuo hivyo. Ada za mafunzo hutofautiana kulingana na gharama za uendeshaji wa kozi husika.

Pia orodha ya vyuo na kozi zinazotolewa pamoja na gharama zake zinapatikana kwenye tovuti ya VETA: www.veta.go.tz