Tathmini Inayozingatia Umahiri (CBA)UtanguliziTathmini Inayozingatia Umahiri (CBA) imeundwa kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa wazi vya utendakazi ambavyo huweka wazi kabisa kile ambacho mwanafunzi anatarajiwa kuweza kufanya. Ili kufaulu kozi inayozingatia uwezo, mwanafunzi lazima aonyeshe ufaulu wa vigezo vyote vya utendaji ambavyo vinahusishwa na umahiri. Kwa sababu tathmini inayozingatia umahiri (CBA) inahusishwa kwa karibu zaidi na uwezeshaji halisi na mchakato wa kujifunza, kwa hiyo tathmini endelevu na tathmini ya mwisho hutumiwa kumpima mwanafunzi. Miongozo imezingatia aina kuu mbili za tathmini yaani tathmini endelevu na tathmini ya mwisho. Tathmini zote mbili zinachukuliwa kuwa tathmini muhimu huchukuliwa kama michakato muhimu ya tathmini katika kubainisha mafanikio ya wanafunzi na watahiniwa katika umahiri. Zaidi ya hayo, miongozo inaainisha vigezo vya utunuku wa vyeti na maelezo ya madaraja jinsi yanavyopaswa kuonekana katika cheti cha umahiri. Miongozo ina sehemu tatu, ambazo zinaakisi makundi makuu mawili ya wanafunzi wanaohitaji Tathmini inayozingatia Umahiri. Miongozo inajumuisha wanafunzi walio katika vyuo vya mafunzo na wanagenzi katika sehemu rasmi za kazi na zisizo rasmi. Kama njia za tathmini zinayozingatia umahiri katika kutathmini ujuzi, maarifa na mtazamo wa watahiniwa kama zilivyofundishwa wakati wa mafunzo. Kinyume na njia nyingine za tathmini, tathmini inayozingatia umahiri kwa kiasi kikubwa ni mbinu ya tathmini inayomhusu mwanafunzi ambaye anahusishwa moja kwa moja katika michakato yote ya tathmini. Tathmini inayozingatia umahiri inaweza kugawanywa katika aina mbili pana ambazo ni Tathmini Endelevu na Tathmini ya mwisho. Utaratibu wa Kujiunga na Kozi za Muda Mrefu Kwenye Vyuo vya VetaVETA imeweka utaratibu na sifa za kujiunga na kozi za muda mrefu kama ifuatavyo: Nafasi za kujiunga na masomo hutangazwa mwezi wa Agosti kila mwaka. Matangazo hutolewa katika vyombo vya habari nchini pamoja na kwenye tovuti ya VETA yaani www.veta.go.tz
Ada na Gharama za MafunzoAda za mafunzo kwa kozi za muda mrefu kwa vyuo vinavyomilikiwa na VETA kwa sasa ni shilingi 60,000/= kwa mwanafunzi wa kutwa katika fani zote na bweni ni shilingi 120,000/=. Gharama zingine hutegemeana na fani na mahitaji mahsusi kwenye chuo husika. Orodha ya vyuo na fani zinazotolewa kwenye vyuo husika zinapatikana kwenye tovuti ya VETA: www.veta.go.tz |